Gianluigi Donnarumma, Mchezaji Bora Euro 2020.

Pengine sio kawaida kuona kipa anatwaa tuzo ya mchezaji bora lakini Gianluigi Donnarumma amestahili tuzo ya mchezaji bora wa Euro 2020.

Akiwa na umri wa miaka 22, Donnarumma amekuwa muhimili imara kwenye goli la Italia kwenye mashindano ya Euro 2020. Kwa mara ya pili, golikipa anatwaa tuzo ya mchezaji bora wa Euro – 1992 alitwaa Peter Schmeichel kwa mara ya kwanza kwenye historia ya mashindano hayo.

Gianluigi Donnarumma amecheza jumla ya dakika 719 kwenye mashindano ya Euro 2020, huu ni muda mrefu zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote kwenye mashindano haya. Donnarumma amemaliza mashindano kwa kutoa hati 3 safi (clean Sheets) ikiwa ni sambamba na kucheza penati 2 (ya Jadon Sancho na Bukayo Saka) kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Uingereza.

Pedri

Sambamba na Gianluigi Donnarumma ambaye muda mfupi atatangazwa kama mchezaji mpya wa PSG akitokea AC Milan. Mchezaji kinda wa Hispania, Pedri amepatiwa tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwenye mashindano ya Euro 2020.

Pedri amekosa dakika 1 tu kwenye michezo yote ambayo Hispania imecheza kwenye mashindano ya Euro 2020. Kabla ya mashindano haya, Pedri alikuwa ameitumikia Hispania mara 4 pekee akiwa na umri wa miaka 18 kwa sasa.

Cristiano Ronaldo

Licha ya kuishia kwenye hatua ya 16 bora, Cristiano Ronaldo (Ureno) ametwaa kiatu cha mfungaji bora (magoli 5) wa Euro 2020. Japokuwa Patrik Schick (Czech Republic) alifunga magoli 5 kama CR7, Ronaldo ameibuka kidedea kwa kuwa na pasi 1 ya goli (vs Ujerumani).


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.