Tetesi zinasema, Tottenham wanaweza kumsajili kiungo wa kati wa Roma Lorenzo Pellegrini, 25, lakini watatakiwa kutoa kititia cha pauni milioni 26 kumnasa Muitaliano huyo.
Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 23 ambaye The blues pia wameashiria kuwa tayari kumuuza kwa Tottenham na Inter milan.
Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anawataka viongozi wa klabu kumsajili mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah,29, anayekipiga Liverpool ikiwa mchakato wa kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe utakwama msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Tottenham wanamtaka mshambuliaji Danny Ings lakini wanakabiliwa na ugumu kwasababu Southampton wanasita kufanya biashara na klabu hiyo ya kaskazini mwa London.
Mabingwa wa Uhispania Atletico Madrid wamekuwa wakihusishwa na taarifa za kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard, ambaye pia anatolewa macho na West Ham ambao walipendezwa naye alipokuwa kwa mkopo msimu uliopita.
Tetesi zinasema, Real Madrid wameridhia kuwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Raphael Varane hatasaini mkataba mpya na wanasubiri ofa ya Manchester United.
Tetesi zinasema, Brentford wanajiandaa kuweka mezani ofa ya ya pauni milioni 13.5 kwa ajili ya mlinzi wa Celtic Kristoffer Ajer,23.
Mlinzi wa Chelsea Emerson Palmieri,26, anatakiwa na Inter Milan na Roma, huku akiwa chaguo pendwa kwa Napoli wakati pia wakimtolea macho Mathias Olivera, 23, anayekipiga Getafe.

Kumsajili mchezaji wa Arsenal Joe Willock,21, kwa mkataba wa kudumu bado imekuwa kipaumbele cha Newcastle United msimu huu baada ya kiungo huyo wa kati, 21, kuwepo St James’ Park kwa mkopo msimu uliopita.
Tetesi zinasema, AC Milan wamekataa zabuni ya pauni milioni 34 kutoka Paris St-Germain kwa ajili ya kiungo wa kati wa Ufaransa Theo Hernandez mwenye miaka 23.
Inter Milan imeisitiza kuwa kiungo wa kati Nicolo Barella HAUZWI baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 24 ataelekea Liverpool na Manchester United.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!


