Bosi wa Paris Saint-Germain Mauricio Pochettino amesema kwamba Lionel Messi atakuwa sehemu ya kikosi kwenye mchezo wa Wikendi inayokuja ambapo PSG itafanya ziara ya kwenda Reims kwa mechi ya Ligue 1.

Baada ya kupata ushindi wa mechi tatu mfululizo za ufunguzi psg sasa wapo juu ya kwenye msimamo wa ligi hiyo na wanazidi kuimarika licha ya kukosekana kwa wachezaji kama Messi na Neymar.
Hiyo haijaleta upungufu wowote zaidi zaidi ni kwamba tajiri anaenda kuwa tajiri zaidi pale wachezaji hao wawili watakapo ungana na timu wakati pia usajili mpya Gianluigi Donnarumma aliweza kukaa benchi kwenye mchezo wa Ijumaa waliyoshinda 4-2 dhidi ya Brest.

“Wiki imekuwa nzuri sana kwa Leo Messi, kwa hiyo tunatumai wiki ijayo inaweza kuisadia timu atajumuishwa kwenye kundi kwaajili ya ushindani,” Pochettino aliiambia ESPN.
Wakati Achraf Hakimi na Georginio Wijnaldum wamecheza michezo yote mitatu ya PSG katika ligi baada ya kujiunga na miamba hiyo ya Ufaransa.
Messi, Donnarumma na Ramos bado hawajaweza kufanya mchezo wowote kwa PSG mpaka sasa na Ramos hatocheza mpaka baada ya mapumziko ya kimataifa.
Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.



Sania+mapua
Piga kazi Messi