Tetesi zinasema, Real Madrid imepeleka ofa ya kwanza ya £137m kwa ajili ya mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22, lakini klabu hiyo ya Ufaransa inatarajia kukataa ofa yoyote kwa ajili ya nyota huyo aliyebakiza mkataba wa mwaka mmoja.
Tetesi zinasema, PSG inaweza kumuwania mshambuliaji wa Everton na Brazil Richarlison, 24, kama mbadala wa Mbappe.
Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 36, anataka kuhamia mabingwa wa ligi kuu England Manchester City katika wiki hili la mwisho la usajili.

Klabu za ligi kuu England Premier hazitawaruhusu wachezaji wake kurejea kuchezea timu zao za taifa katika mataifa yenye hatari kubwa ya maambukizi ya korona.
Tetesi zinasema, Manchester United wako katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland msimu ujao.
Tetesi zinasema, Chelsea huenda inachuana na Manchester United kutaka kujaribu kunasa saini ya kiungo wa Atletico Madrid na Hipsania Spain Saul Niguez, 26, kwa mkopo.
Arsenal imefanya mazungumzo na Atletico Madrid kuhusu uhamisho wa beki wa kulia wa England Kieran Trippier, ingawa beki huyo mwenye miaka 30 angetamani kwenda Manchester United kama atatakiwa kuondoka Madrid.

West ham pia wana matumaini ya kumsajili mlinzi wa kati wa Ufaransa Kurt Zouma kutoka Chelsea baada ya jaribio la kumsajili mlinzi huyo mwenye miaka 26 kwenda vyema.
West Ham wanaangalia pia uwezekano wa kumsajili winga wa CSKA Moscow na Croatia Nikola Vlasic, 23, kama mbadala wa kiungo mshambuliaji wa England Jesse Lingard, 28 kutoka Manchester United ambaye anatarajia kubaki Old Trafford.
Mawakala wa mchezaji wa kimataifa wa uholanzi Donny van de Beek, 24 wamepuuzilia mbali timu zilizoonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo ambaye anataka kupambania namba Manchester United.
Mlinzi wa kulia wa Liverpool na Wales Neco Williams huenda akasalia Anfield baada ya mbio za vilabu vinavyomuwania kinda huyo mwenye miaka 20 kufifia katika wiki za karibuni.

Ofa ya Burnley ya £15m kwa ajili ya mlinzi wa kushoto wa Ivory Coast Maxwel Cornet imekubaliwa na klabu yake ya ufaransa Lyon na sasa mpira upo kwa nyota huyo mwenye miaka 24 kama atataka kujiunga na kikosi hicho cha Turf Moor.
Kiungo wa Uruguay Federico Valverde, 23, amekubali mkataba mpya utakaombakiza Real Madrid mpaka mwaka 2027 wneye kipengele cha malipo ya £856m kama atauzwa.
Tetesi zinasema, Mlinzi wa Barcelona Sergi Roberto, 29, na kiungo mwenye umri wa miaka 33 Sergio Busquets, wanatarajia kukubali kupunguza mishahara na kusalia kwenye klabu hiyo ya Laliga.
Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.



Sarah
Ziko vizuri