Saul Niguez wa Atletico Madrid Anukia Chelsea

Chelsea ni miongoni mwa vilabu vilivyopewa nafasi ya kumsajili kwa mkopo kiungo wa Atletico Madrid, Saul Niguez.

Saul Niguez wa Atletico Madrid Anukia Chelsea

Saul alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda taji la Diego Simeone msimu uliopita lakini ataruhusiwa kuondoka klabuni msimu huu wa joto.

Mchezaji huyo wa miaka 26 ameichezea Atletico zaidi ya mechi 300 tangu alipoingia kwenye kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 17 mwaka 2012.

Amecheza pia mara 19 kwa timu ya taifa ya Uhispania lakini aliachwa kwenye kikosi chao cha Euro msimu huu wa joto.

Manchester United wamekuwa wakimtolea macho kiungo huyo, pamoja na Eduardo Camavinga kutoka Rennes.

Kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel alisema Jumapili alikuwa na furaha na kikosi chake lakini, anaweza kutafuta kusaini kiungo mwingine baada ya kumruhusu Billy Gilmour ajiunge na Norwich City kwa mkopo.

Tuchel tayari ana chaguzi kadhaa za kiungo ikiwa ni pamoja na Jorginho, Mateo Kovacic na N’Golo Kante.

Chelsea wanajaribu kutafuta vilabu vinavyo taka viungo wa kati Tiemoue Bakayoko, ambaye yuko karibu kujiunga na AC Milan kwa mkopo, Ross Barkley na Danny Drinkwater.

Chelsea inafanya mazungumzo na wawakilishi wa mlinzi Antonio Rudiger juu ya mkataba mpya.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa sasa lakini alimwambia Tuchel bado anajitolea kabisa kwa klabu ya EPL.


NAMBA 40 ZA MKWANJA

Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

2 Komentara

    Mhh ngoja tuone

    Jibu

    Tunasubiri tuone

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.