Thiago Silva amekiri kwamba alihuzunika Paris Saint-Germain kufanya uamuzi wa kumsajili Sergio Ramos kwani hakupata ofa kama hiyo licha ya wawili hao kutopishana sana umri.

Nahodha wa zamani wa Real Madrid ni mmoja ya wachezaji waliyo sainiwa na PSG katika dirisha la usajili linalokwenda kufungwa wiki ijayo.
Silva ambaye ameingia kwenye mwaka wa pili huko Stamford Bridge amesema kwamba hana tatizo na Ramos lakini yeye aliitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu na kwa kujitolea kwa asilimia mia.
“Sina tatizo na Sergio Ramos, Ramos kwa muda ambao wamempa ofa ya kumsajili kwa miaka miwili umri ambao nilikuwa nao msimu uliyopita. Silva mwenye umri wa miaka 36 aliiambia ESPN Brazil.
“Kwa hiyo ilinifanya niuzunike kweli, sijaongea na mtu yoyote kuhusu hili sababu inafanya nijihisi kuhuzunika inafanya nijihisi kama sikufanya chochote katika klabu.
Unawezaje kuikosa hii! Ndani ya kasino za meridianbet kuna mchezo unaoweza kukupa mkwanja mrefu leo hii, Wild Hot 40 ni njia nyingine ya kukufanya milionea, Chagua namba yako na uvune mkwanja.


