Chelsea hawajafanikiwa kukamilisha mazungumzo ya mkataba mpya wa Antonio Rudiger.
Klabu ya Chelsea inaripotiwa kuwa inakutana na kikwazo, katika jitihada za kumshawishi nyota wake Antonio Rudiger kusaini mkataba mpya.
Mlinzi huyu wa kati, mwenye uraia wa Ujerumani -ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu chini ya Thomas Tuchel- tayari ameingia kwenye miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja huko Uingereza, ofa ya hivi karibuni ya Chelsea ya mkataba mpya wa Antonio Rudiger ilienda tofauti, huku maboresho zaidi yakishauriwa kufanyika kwenye mkataba huo.

Taarifa zinasema kuwa hali ya mkataba wa nyota huyu, mwenye miaka 28 inafuatiliwa na vilabu kadhaa vikubwa wakiwemo Real Madrid, Bayern Munich, Paris Saint-Germain, Juventus na Atletico Madrid.
Pia Tottenham Hotspurs, ndiyo wanatajwa kuwa wapinzani pekee wa EPL wanaojaribu kuonesha nia ya kumtaka staa huyu. Awali Spurs walishajaribu kuinasa saini yake.
Wakati seke seke la mkataba mpya wa Antonio Rudiger zikiendelea, mpaka sasa staa huyu amecheza zaidi ya mechi 150 na Chelsea tangia alipowasili klabuni hapo mwaka 2017.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.



[email protected]
Safi sana