Liverpool Wakaribia Kumnasa Luis Diaz

Liverpool wanandelea kukiimarisha kikosi chao Januari hii sasa wamekaribia kumsajili mchezaji nyota wa Porto na timu ya taifa ya Colombia Luis Diaz kwa dau la awali la Euro milioni 40.

Liverpool Wakaribia Kumnasa Luis Diaz

Mapema siku ya leo, habari zilienea kwamba raia huyo wa Colombia ambaye kwa sasa yuko kwenye majukumu ya kimataifa huko Amerika Kusini alikuwa anatarajiwa kuwa mchezaji mpya wa Majogoo wa Anfield.

Chapisho la Ureno la O Jogo lilisema kuwa makubaliano yamefikiwa kati ya vilabu hivyo viwili, na mpango huo unatazamiwa kufikia euro milioni 60.

Luis Diaz yupo tayari kuachana na klabu inayoshindania mafanikio katika ligi yao ya nyumbani na Ligi ya Mabingwa, huku Liverpool ikionekana kuwa mahali pazuri zaidi.

Hatua hiyo inaweza kufanywa rasmi mara moja, na Mcolombia huyo anaweza, kuingia kwenye kikosi cha Jurgen Klopp baada ya mapumziko ya kimataifa, na kuongeza moto zaidi katika kinyang’anyiro cha EPL

Tottenham walikuwa wamevutiwa na mchezaji huyo lakini sasa wanaonekana kuzidiwa nguvu na Liverpool kwenye usajili wake.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.