Klabu ya PSG walifanya kufuru kwenye dirisha la usajili majira ya joto, 2021/22. Wachezaji huru ndio zilikuwa tageti za klabu hiyo.
Lionel Messi, Gini Wijnaldum, Donnarumma na Sergio Ramos wote walisajiliwa kama wachezaji huru huku wakitoa €60M kumsajili Hashraf Hakimi.
2022/23, PSG wataendelea walipoishia msimu uliopita. Kwenye nafasi ya kwanza kwenye orodha yao ni Paul Pogba. Pogba anamaliza mkataba wake na Manchester United msimu huu, ifikapo July 1,2022 atakua ni mchezaji huru na hivyo, anaweza kujiunga na timu yeyote.
Usajili wa Pogba utaendana na kuondoka kwa Kylian Mbappe ambaye anahusishwa na Real Madrid mwishoni mwa msimu huu.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.