Taarifa zinaeleza kuwa bondia Israel Adesanya amesaini mkataba mpya na MMA unaomfanya kuingia kwenye orodha ya mabondia wanaolipwa pesa nyingi zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa, bondia huyu anakuwa mpiganaji wa pili kati ya wanaovuta mkwanja mrefu zaidi kwenye historia ya ndondi mchanganyiko – Martial Arts, baada ya Conor McGregor anayeshikilia nafasi ya kwanza.
Israel, ambaye amekuwa bingwa wa middleweight mara kadhaa bila kuangushwa, amesaini mkataba wa mapambano mengi na viongozi wa MMA mapema wiki hii.

Hata hivyo, thamani ya dili hilo haitawekwa wazi kwa sasa mpaka atakapoingia kwenye pambano ambalo kiutaratibu litalazimu suala hilo kuwekwa wazi.
Tamko kutoka kampuni ya The Last Stylebender inataja kuwa hilo linakuwa ni dili lenye thamani kubwa kuwahi kutokea kwenye historia ya kampuni hiyo.
“Adesanya, kama matokeo ya dili hili, atakuwa mmoja wa wanamichezo wanaolipwa pesa nyingi zaidi katika historia ya sanaa ya ndondi mchanganyiko.” – imetaja sehemu ya taarifa ya kampuni katika kutangaza mkataba huu.
Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.


