UEFA wamepanga kuwafungulia mashitaka mmiliki wa klabu ya Paris Saint-Germain Nasser Al-Khelaifi na mkurugenzi wa michezo Leonardo pia na klabu baada ya siku ya jumanne usiku kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Real Madrid.
Kulingana na vyanzo vya taarifa, Al-Khelaifi na Leonardo walikwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo referees kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu na kulalamikia goli la kwanza, ambapo wanaamini kuwa golikipa Gianluigi Donnarumma alifanyiwa madhambi.

Inaeleweka kwamba UEFA hawatalifumbia macho na kamati ya maadili na nidhamu watafanya maamuzi haraka iwekanavyo.
“Hatupaswi kutupa kila kitu kwenye pipa la taka,” Leonardo aliliambia RMC Sport baada ya mechi. “Hatuwezi kuanza mwanzo kila baada ya kupoteza, nia yetu ni kuchukua ubingwa wa ulaya, na mpaka kipindi cha kwanza tulikuwa vizuri.
“Inabidi tuangalie jinsi ya kuiboresha hii timu na kudumisha hamasa ya kucheza kwenye Ligue 1 na kumaliza msimu vizuri, inabidi tukae pamoja.
“Pochettino bado yupo kwenye sehemu ya mpango wetu kwenye msimu huu. sio muda wa kufikilia kuhusu hilo.”
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


