Manchester City Wafanya Maamuzi kwa Haaland?

Manchester City wanaripotiwa kufikia makubaliano ya kumleta mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland pale Etihad msimu huu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway anatarajiwa kuwa katikati ya mzozo mkubwa wa uhamisho mwishoni mwa msimu huu, huku kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 63 katika mkataba wake wa Dortmund kikianza kutumika miezi michache ijayo.

Haaland Kwenda Manchester City

Man City inachukuliwa ni moja ya wanaopigiwa upatu zaidi kuipata saini ya Haaland, lakini Real Madrid, Manchester United, Barcelona, ​​Chelsea, Paris Saint-Germain na Bayern Munich pia wanahusishwa.

Hata hivyo, gazeti la Daily Mail linadai kuwa Manchester City yupo mbioni kupata saini ya Haaland, huku mabingwa hao wa Ligi ya Premia sasa wakitarajia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuchagua dimba la Etihad.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa ada za wakala Mino Raiola na bonasi ya kusaini zinaweza kuchukua jumla ya takribani zaidi ya pauni milioni 100, na bodi ya Man City sasa iko tayari kuruhusu zoezi wa uhamisho huo.

Haaland, ambaye baba yake Alf-Inge Haaland aliwahi kuichezea Manchester City hapo awali, amefunga mabao 80 na asisti 21 katika mechi 79 akiwa na Dortmund tangu awasili kutoka Red Bull Salzburg Januari 2020.

 

VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.