Habari njema kwa mashabiki wa Manchester United. Amad Diallo arasimishwa kama mchezaji wa timu hiyo.
Diallo alisajiliwa na United mwishoni mwa mwezi Oktoba lakini kutokana na taratibu za usajili kutokukamilika kwa muda, Amad Diallo aliendelea kubaki Atalanta wakati utaratibu wa kukamilisha usajili ukiendelea.
Baada ya kupatiwa nyaraka muhimu za kumtambua kama mchezaji halali wa The Red Devils, klabu hiyo imemtangaza rasmi mchezaji huyo na punde atajiunga na wachezaji wengine muda mfupi baada ya kupatiwa Visa.

Akiwa Atalanta, Diallo amecheza michezo 5 ya kikosi cha kwanza akiwa amepachika goli 1 pekee. Uwezo wake uwanjani unamfanya kinda huyu kufananishwa na Lionel Messi akiwa na umri wa miaka 18 kwa sasa.
Diallo amesaini mkataba wa miaka 5 ambao unaweza kuongezwa mwaka 1 wa ziada na huenda akapatiwa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza chini ya Ole Gunnar Solskjaer.
Ndio, kwetu Mteja ni mfalme. Jiunge sasa na familia ya Meridianbet bila malipo yeyote na sisi tutakuzawadia bonasi ya shilingi 3,500 kama sehemu ya kukukaribisha kwenye familia hii BURE!!!. Unasubiri nini??



Shakila mrope
Karibu san amadi dialo
David Pere
Akiwa Atalanta, Diallo amecheza michezo 5 ya kikosi cha kwanza akiwa amepachika goli 1 pekee. Uwezo wake uwanjani unamfanya kinda huyu kufananishwa na Lionel Messi akiwa na umri wa miaka 18 kwa sasa.
Adelta
Amad Diallo anakubalika na Yuko vizuri kwenye mpira
Sania
Hongera Amad Diallo
Magdalena
Kila la kheri amad
Hopemwaikuka
Kapge kaz kijana
Lydia Emmanuel Magoti
Habari nzuri kwa Man U
Gabriel
Habar njema
Sabrina
Amad diallo anakuja kukiwasha man u
Sarah
Mambo mazuri kwao man u
Rahmal
Hamadi diallo kalibu sana
Mwanahamisi
Habari njema
Sylvester
Diallo itabidi apambane sana ili aweze kuingia kikosi cha kwanza kwani kule mbele naona kutakua na upinzani mkubwa sana
Dorophina
Habari njema kwa mashabiki lkn kijana inabidi ajaze buti
Caroline
Hongera sana
lombo
Saf
Angelina
Kila la kheri
aisha
Kila la kheri amad
Issa
Dialo. Njoo huku united
warda
Amadi katua pindi sahihi