Barcelona Bado Wapo Kwenye Mbio za Ubingwa

Baada ya Barcelona kuilaza Real Madrid kwa mabao 4-0 siku ya Jumapili sasa tunaweza kuwaweka katika mbio za kusaka ubingwa wa LaLiga licha ya kuachwa alama 12 na viongozi Los Blancos.

Mabao ya Barca yalifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang ambaye aliweka kambani mara mbili, Ferran Torres na Ronald Araujo.

Real Madrid wanaongoza jedwali la LaLiga kwa alama 66 baada ya michezo 29 wakati Barca wao wana alama 54 katika michezo 28 wakiwa nafasi ya tatu nyuma ya Sevilla ambao wana alama 57.

The Blaugrana sasa hawajafungwa katika michezo 10 mfululizo ya LaLiga na wameshinda mechi tano mfululizo baada ya kuifunga Real Madrid.

“Sijui kama tutashinda taji lakini hatuwezi kutoa chochote,” Xavi alisema baada ya mechi kumalizika “Labda tumechlewa kidogo lakini huu ni ushindi mkubwa kwetu sisi.”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe