Mashine ya mabao ya Manchester City Erling Haaland amefichua lishe inayomfanya apendeze, ambayo ni pamoja na moyo, ini na maji yaliyochujwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ameianza Ligi ya Uingereza kwa moto mkali tangu ahamie Uingereza msimu wa joto.
Tangu awasili kutoka Borussia Dortmund kwa £51m, amefunga mabao 20 huku umbile lake la ajabu likimsaidia kutawala safu ya ulinzi.
Na mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway ametoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wake wa mtindo wa Hannibal Lecter ‘kupendelea nyama’ katika waraka wake wa hivi karibuni unaoitwa ‘Haaland: The Big Decision’.
“Nyinyi (watu wengine) hamli hii, lakini ninajali kutunza mwili wangu,” Haaland alisema huku akionyesha vipande vikubwa vya moyo na ini kutoka kwa mchinjaji wake.
“Nadhani kula chakula bora ambacho ni cha kawaida iwezekanavyo ni muhimu zaidi. Watu wanasema nyama ni mbaya kwako lakini ipi? Nyama unayopata McDonald’s? Au ng’ombe wa kienyeji anakula nyasi pale pale? Ninakula moyo na ini.”
Pia alidai yeye hunywa maji tu yaliyochujwa vizuri.
“Kitu cha kwanza ninachofanya asubuhi ni kupata mwanga wa jua machoni mwangu, pia nimeanza kuchuja maji yangu kidogo. Nafikiri inaweza kuwa na faida kubwa kwa mwili wangu.”