makocha wengi wa soka wakiendelea kukosa umaarufu ikilinganishwa na wachezaji wao ,Makocha ni kiungo muhimu katika kubaini hatma ya timu uwanjani.

Makocha huchukua jukumu la kuwa washawishi .Ndio wanouhusika na kuwafunza wachezaji kufikia kiwango cha juu cha mchezo.

Makocha Ndio wenye jukumu la kutathmini wapinzani na kutafuta mkakati wa kupata ushindi. Ili kufikia kiwango kizuri cha mchezo , klabu kubwa hutafuta wakufunzi bora ili kusimamia klabu hizo.

Hatahivyo Makocha bora pia huzigharimu timu zinazowasaka. Katika miongo miwili iliopita baadhi ya makocha wameanza kupokea fedha nyingi zaidi ya wachezaji wao.

Hivyobasi bila kupoteza wakati tuwaangazie makocha kumi tajiri zaidi duniani 2021.

10. Rafael Benítez – Ana thamani ya €13M

Raphael Benitez

Rafael Benítez

Mkufunzi huyo wa zamani wa Real Madrid na Liverpool yupo katika nafasi ya 10 katika orodha ya makocha tajiri zaidi duniani. Kwasasa anaifunza klabu ya Dalian Proffessionals. Huku akipokea mshahara wa €13M, mkufunzi huyo wa Uhispania yupo katika nafasi ya 10.

9. Massimiliano Allegri – Ana thamani ya €13.5M

Allegri

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Allegri ni miongoni mwa wakufunzi tajiri duniani.

Massimiliano “Max” Allegri ni mchezaji wa zamani wa Itali , ambaye mara ya mwisho aliifunza klabu ya Juventus .

Allgeri alikuwa kiungo wa kati aliyechezea klabu tofauti nchini Itali. Akiwa na mapato ya jumla ya €13.5M na thamani ya $5m, Massimiliano Allegri ameorodheshwa katika orodha ya wakufunzi 10 bora duniani.

8. Fabio Cannavaro – ana thamani ya €14m

Canavaro

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Fabio Cannavaro ni mmoja ya Makocha tajiri zaidi duniani.

Akiwa na thamani ya $45 Million, Cannavaro ni miongoni mwa wakufunzi tajiri duniani. Kandarasi yake kwa sasa inamsaidia kujipatia €12m kwa mwaka. Chini ya usimamizi wake Klabu hiyo ya China imefanikiwa kushinda kombe la China la FA 2018 na ligi ya China 2019.

7. Ernesto Valverde – Ana thamani ya €19M

Ernesto

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ernesto Valverde

Ernesto Valverde Tejedor ni mchezaji wa mpira wa zamani wa Uhispania ambaye alicheza kama mshambuliaji na sasa ni mkufunzi.

Ernesto alishinda mataji mawili na klabu ya Olympiacos 2008-09 na 2011-12 na Barcelona 2017-18. Valverde alifutwa kazi mwaka huu baada ya msimu mbaya na Barcelona , baada ya kupoteza kwa Bayern Munich 8-2.

6. Zinedine Zidane – ana thamani ya €23M

Zidane

Zidane ni mongoni mwa mameneja 10 tajiri zaidi duniani. Kwa jina maarufu Zizou ni mchezaji wa zamani wa Ufaransa.

Akiwa mkufunzi amekuwa akipokea €23M kwa mwaka na ana thamani ya €62m, thamani inayomfanya kuwa miongoni mwa wakufunzi tajiri zaidi duniani.

Pia anashikilia rekodi ya kushinda mataji matatu ya klabu bingwa akiwa mkufunzi.

5. José Mourinho – Ana thamani ya €23M

Jose Mourinho

Jose Mourinho amejishindia mataji mengi akiwa mkufunzi baada ya kushinda mataji sita katika misimu miwili. Mkufunzi huyo wa Uareno amekuwa akipokea €23M na thamani yake kwa jumla inadaiwa kuwa kati ya $50m – $100m, thamani inayomfanya kuwa mmoja wa mameneja tajiri zaidi duniani.

4. Jürgen Klopp – Ana thamani ya €24M

Jurgen Klopp

Jurgen Klopp

Jürgen Norbert Klopp ni raia wa Ujerumani na mchezaji wa zamani ambaye ndiye meneja wa Liverpool .

Jurgen Klopp ana thamani ya $50million, thamani inayomfanya kuwa miongoni mwa makocha tajiri England .

3. Pep Guardiola – Ana thamani ya €27M

Pep Guardiola

Guardiola ndiye mkufunzi tajiri zaidi England . Josep ”pep” Guardiola Sala ni raia wa Uhispania na mchezaji wa zamani ambaye ndiye mkufunzi wa sasa wa klabu ya Manchester City.

Ana sifa za kuwa mkufunzi aliyefanikiwa zaidi duniani, Akiwa mchezaji , Pep alihudumia wakati wake mwingi akiifuna Barcelona . Akiwa mkufunzi ,Pepe amejishindia mataji chungu nzima akifunza klabu tofauti.

Anapokea €27M kila mwaka kama meneja wa Manchester City na thamani yake ni kati ya $40-60 m hatua inayomfanya kuwa mkufunzi tajiri zaidi England

2. Antonio Conte – Ana thamani ya €30M

Makocha

Antonio Conte

Antonio Conte ni mkufunzi wa Itali na mchezaji wa zamani.

Ndiye kocha mkuu wa InterMilan . Ana sifa za kutumia mbinu ya 3-5-2 katika kipindi chake cha ukufunzi . Aliisaidia InterMilan kufika fainali za kombe la Yuropa katika msimu wake wa kwanza ambapo timu yake ilishindwa na Sevilla katika fainali.

Conte anapokea €30M kila mwaka na thamani yake inadaiwa kuwa kati ya $50-60m

1. Diego Simeone – Ana thamani ya €40.5m

Makocha
Diego Simione

Diego Simeone ndiye mkufunzi tajiri zaidi duniani.

Anapokea €40.5M kila mwaka. Pia ni miongoni mwa wakufunzi wanaopokea fedha nyingi z aidi duniani 2021. Raia huyo wa Argentina amefunza klabu kadhaa lakini amepata ufanisi mkubwa akiifunza Atletico Madrid , kwa kuisaidia kushinda taji la La Liga, Copa del Rey, makombe mawili ya Yuropa, makombe mawili ya UEFA Supercup na kuwa katika nafasi ya pili katika kombe la klabu bingwa Ulaya .

Thamani ya Diego Simeone inadaiwa kuwa $130m kulingana na mtandao wa Celebrity net worth na hivyo kuwa mkufunzi tajiri zaidi duniani.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa