Marcelo Kuwa Nahodha wa Kwanza wa Kigeni Real Madrid

Beki wa Real Madrid Marcelo amekuwa nahodha wa kwanza ambaye siyo mtaifa wa Uhisapania tangu mwaka 1904 baada ya Madrid kuachana na aliyekuwa nahodha wao Sergio Ramos.

Marcelo Kuwa Nahodha wa Kwanza wa Kigeni Real Madrid

Kwa matokeo hayo Marcelo anakuwa nahodha wa Real Madrid kwa msimu unaokuja tangu alipokuwa Federico Revuelto wa Guatemala miaka 117 iliyopita.

Kwa utamaduni wa Real Madrid unahodha anapewa mchezaji aliyedumu na timu kwa muda mrefu, hii inamaanisha Mbrazil ambaye amekuwa na Madrid kwa takribani miaka 15 atakabidhiwa kitambaa cha unahodha.

Na kitambaa hicho kitakuwa kikivaliwa na Karim Benzema pale Marceloa asipokuwepo uwanjani kwakuwa yeye anamfuatia Marcelo kwa kukaa muda mrefu huko Bernabeu.

Tangu alipokuwa nahodha wa timu mwaka 2015 akirithi kutoka kwa Iker Casilas, Sergio Ramos ameiongoza timu kupata mafanikio mengi kwa kushinda mataji 12 yakijuishwa mataji matatu mfululizo ya Champions League kutoka mwaka 2016 mpaka 2018.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

Acha ujumbe