Shirikisho la mpira wa miguu nchini Urusi limejibu mapigo kwa kupinga maamuzi yaliotolewa na FIFA na UEFA kuwaondoa kwenye mashindano yote yanayoandaliwa na taasisi hizo wakidai kuwa hawana haki ya msingi kuwazuia kushiriki mashindano hayo.

Vyama hivyo vya soka duniani na Ulaya vyote vimechukua hatua ya kuziondoa timu zote za Urusi kwenye mashindano hayo, baada ya serikali ya nchi hiyo kufanya uvamizi wa kijeshi kwenye nchi ya Ukraine.

Urusi

UEFA ndio ilianza kuiondoa nchi ya Urusi kwenye mashindano yake na kuziondoa timu zote za Urusi, huku Spartak Moscow ikikumbwa na kadhia hiyo kwa kuondolewa kwenye ligi ya Europa League, kwa hatua za haraka.

FIFA walianza kwa kuiwekea vikwazo kidogo, kabla kuindoa kabisa baada ya nchi wanachama kugoma kucheza na nchi  hiyo kwenye michezo ya kufuzu kombe la Dunia, hii inamaanisha kuwa Urusi haitaweza kucheza michuano ya kombe la Dunia nchini Qatar kwenye majira ya baridi.

Chama cha soka nchini Urusi kilitoa waraka ambao ulionesha kutokuridhishwa na kuzuiwa kwao, huku wakidai ni uvunjifu wa haki yao ya msingi,imevunja haki ya msingi ya RFU kama mwanachama wa FIFA na UEFA, ikiwemo haki ya kushiriki mashindano.

“Maamuzi ya kuiondoa timu yetu kwenye michezo ya kufuzu kombe la Dunia 2022, ilikuwa shinikizo la nchi ambazo ilikuwa inabidi tucheze nazo michezo ya kufuzu ambapo ni kinyumea na sheria ya michezo huru kwa wote.

“Pia shirikisho la mpira wa miguu Urusi halikupewa nafasi, ambapo ni kinyune na sheria na haki ya msingi ya kujitetea.”


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa