Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi ameripotiwa kukutana kwa siri na mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Erling Braut Haaland jijini Munich ili kumushawishi aweze kujiunga na klabu hiyo kwenye majira ya kiangazi.

Barcelona imekuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu mshambuliaji huyo huku klabu kubwa zingine nazo zikiwania saini yake, ambapo kifungu cha kuvunja mkataba wake kina thamani ya €75 million huku mpaka anaondoka Dortmund inakadiliwa itakuwa ni €110 million ambapo hiyo itajumuisha kamisheni ya wakala wake na baba yake.

Xavi
Xavi

Xavi hataki kuikosa saini ya mshambuliji huyo ambapo repoti zinasema kuwa kwenye safari ya siri waliyofanya kwenda Munich siku ya jumanne akiwemo raisi wa klabu Joan Laporta, mshauri Jordi Cruyff ilikuwa ni kwa sababu ya kufanya kikao na Haaland.

Baada ya Mundo Deportivo, kutoa siri hiyo klabu haikuweza kukanusha kuwa walisafiri kwenda Ujerumani, japokuwa Jordi Cruyff alisema kuwa yeye alisafiri kwenda London, huku ikibaki sintofahamu kwa Xavi na rais wa klabu hiyo kuhusu safari yao.

Wiki iliyoisha kulikuwa na taarifa kuwa Joan Laporta alifanya safari ya kwenda Monaco kuongea na Mino Raiola mwenyewe, kuhusu uhamisho wa beki wa kulia wa timu ya  Ajax, Noussair Mazraoui na Haaland kwa pamoja.

Pia kuna taarifa njema kuwa kwenye hivi vikao viwili kuna uwezekano mkubwa wa klabu ya Barcelona kuweza kupata saini ya Haaland, japo lolote linaweza kutokea baada ya mahasimu wao Real Madrid nao kuhitaji saini ya mshumbuliaji huyo.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa