Rose Atamani Kurudi Spurs.

Danny Rose anapenda kupata fursa ya kucheza mbele ya mashabiki wa Tottemham kwa mara nyingine na atafurahi kama atamaliza muda uliyobaki katika mkataba wake akiwa na Spurs.

Beki wa kushoto wa England Rose ametumia nusu ya msimu wa 2019-20 katika Premier League kucheza katika klabu ya Newcastle kwa mkopo baada ya kutokuwa chaguo la kocha Jose Mourinho pindi alipochukua nafasi ya Pochettino kuinoa Spurs mwezi Novemba mwaka uliyopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 aliiambia BBC Radio 5 Live anajihisi “Hakupewa nafasi kubwa ya kucheza kama watu wengine katika safu ya ulinzi” na kocha Mourinho.

Rose yupo kwenye mkataba na timu ya Tottenham mpaka mwaka 2021 mwezi Juni na aliiambia The Second Captains amekuwa akitamani kufufua matumaini ya kuendelea kucheza katika klabu hiyo.

“Nitafurahi kukaa Tottenham na kuona miezi 10-11 iliyosalia naimalizia hapo,”

“Hakuna chochote ninachokihitaji zaidi ya kucheza nahitaji kucheza mbele ya mashabiki Spurs.

“Mechi yangu ya mwisho kucheza nikiwa na Tottenham ilikuwa ni dhidi ya Liverpool tulipoteza kwa 1-0 sikujua kama ndiyo mchezo wangu ma mwisho klabuni.”

Rose alishawahi kuhusishwa na kuhamia Manchester United, alikuwa ni beki mchezeshaji chini ya kocha Pochettino pia alikuwa ni sehemu ya timu ya England mwaka 2018 walipofika hatua ya nusu fainali katika michuano ya kombe la dunia.

Rose alifunga goli dhidi ya Arsenal mwaka 2010 katika Premier League na ameichezea Spurs michezo 210 katika mashindano yote.


Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.

Ingia mchezoni

40 Komentara

    Anamapenzi na team

    Jibu

    Rose mchezaji mzuri

    Jibu

    rose majeruh ndo yamemfany kupotezah namba spur na kupelekea kutolew kwa mkopo Ila natumain atafany vzr atarud Tena kuchez na Uzi wa spur kikubw jitihad na maarifa haongezeh huko alipo thnk meridian bet tz kwa update

    Jibu

    Kiukweli rose asikiki kabisa saivi majeruhi ya Mara kwa Mara ndilo tatizo kwake.

    Jibu

    Asante meridianbet kwa taarifa

    Jibu

    Kama kuna kulipa rud tu

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Arudi tu kama anaona masirahi yapo spurs

    Jibu

    Harudi tyuu Spurs akakipige

    Jibu

    New updates.

    Jibu

    Habari njema.

    Jibu

    Kama masilah yapo wewe rud

    Jibu

    Arudi tu

    Jibu

    Majerui ndo yamemfanya apoteze dira uyu jamaa

    Jibu

    Habari njema hii itakuwa poa sana rose akirudi spurs kuichezea klabu yake

    Jibu

    Rose acha kuhangaika unatakiwa utulie sehemu moja ili utengeneze mafanikio yako ya baadae kwasababu mpira unamwisho huwezi kucheza milele

    Jibu

    Bora rose arudi kwenye timu tu

    Jibu

    Daah rose yupo nishamsahau kabisa kijana mjeuri ambaye anajituma ila wakati mwingine anafanya ujeuri mpaka anapotea apunguze utoto abadilike ili ndoto zake zitimie

    Jibu

    Akirud itakuwa vizuri

    Jibu

    Rose yupo vizuri sana majeraha aliyokua nayo ndio yanayo mfanya ashuke kwa kiwango chake alichokua nacho tunamatumaini hatakua na hujio mpya msimu huu

    Jibu

    Arudi tu

    Jibu

    Kama bado kiwango anacho arudi tu maana Hali ni Tete pale anaweza kuisaidia

    Jibu

    you are welcome

    Jibu

    Arudi tuu

    Jibu

    Rudi kama panafaa

    Jibu

    Vizuri Kama anaitaji timu haludi tuu anamapenzi nayo Spurs

    Jibu

    Dan rose mbona ni mchezaji mzuri tuu sema ndo hivo siyo chaguo la mourinho

    Jibu

    Itakuwa jambo zuri akiludi spurs danny rose

    Jibu

    Mourinho anatakiwa kumrudisha Rose kuokoa jahazi sio mchezaji mbaya

    Jibu

    Ongeza juudi urudi spurs.

    Jibu

    Angalia maslai yako

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Rose kufanya hivyo ni sawa na kula matapishi yako

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Aende tu spurs bado wanamuhitaji

    Jibu

    Arudi tu

    Jibu

    Ndo aombe tu Nafasi kipendacho roho #Meridianbettz

    Jibu

    Bado Mourinho ambaye hakumuhitaji yupo Tottenham, nadhani anatakiwa kufikiria kuendelea na mipango mingine nje ya Tottenham#meridianbettz

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.