Mshambuliaji mpya wa Yanga Lazarous Kambole amesema kuwa kwa jinsi anavyotamani kuanza kuitumikikia timu yake hiyo ni kama msimu uanze kwani amejiandaa kufanya vyema ndani ya timu hiyo katika michuano yote ambayo watacheza msimu ujao.

Yanga tayari imeshamtangaza mshambuliaji huyo ambapo ndio ulikuwa usajili wa kwanza kwa Yanga kutambulishwa msimu huu akitokea katika klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini.

Kambole alisema kuwa anatamani kuona msimu ukianza mapema kutokana na hamu kubwa aliyonayo kuanza kuitumikia timu yake mpya ya Yanga ambapo matumaini makubwa kwake ni kuona anafanya vyema ndani ya Yanga.

“Natamani ligi ianze mapema hivi karibuni kutokana na kuwa na shauku ya kuanza kuitumikia Yanga katika michuano ya msimu ujao ya ligi na kimataifa ambayo tutashiriki.”

“Malengo yangu ni kuhakikisha kuwa nafanya vizuri zaidi nikiwa na Yanga kwa kuwa ni timu ambao imeonyesha kuwa inamalengo makubwa ya kufanya vizuri kwa msimu ujao na ndio maana nataka kuwa sehemu ya historia hiyo ya Yanga kwa msimu ujao,” alisema mchezaji huyo”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa