Kampuni ya Puma imeomba radhi kwa makosa waliyofanya katika utengenezaji wa jezi ya tatu ya Borussia Dortmund kwa kutoweka nembo ya klabu na kupelekea wachezaji kushindwa kuibusu jezi wakati wakishangilia na mashabiki hawana furaha na hilo.

Kampuni hiyo ya mavazi ya michezo imelazimika kuomba radhi kwa mashabiki wa Borussia Dortmund.
Katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Besiktas ambao Dortmund walitingia jezi ya tatu kwa mara kwanza msimu huu ambayo imepambwa na rangi ya njano ambayo imekuwa na muundo kama wa msimu wa 1997/1998 lakini mashabiki wameipinga vikali kwa kutokuwa na nembo ya klabu.
“Tunajutia hasira za mashabiki na tungependa kuomba radhi kwa hilo,” Mkurugenzi wa Puma Bjorn Gulden alisema.
Borussia Dortmund walijaribu kurekebisha suala hilo wenyewe, wakiweka stempu ya kuhamisha nembo kwenye kila fulana, lakini suluhisho hili halikufanya kazi kwani haikuwa rangi ile ile, zaidi ya hapo klabu haikuweza kutumia jezi lingine kwani walikuwa wamesajiliwa tayari uteuzi wao na UEFA.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


