OFISA Habari wa Mashujaa FC inayoshiriki michuano ya Championship, Benson Mwangatwa amesema kuwa tetesi zinazoendelea kuhusiana na Kocha Msaidizi, Abdi Kassim ‘Babi’ kuondoka sio za kweli na bado yupo sana.
Akizungumzia hilo Mwangatwa amesema “Kuna tetesi zilienea sana hasa kwa mashabiki na wadau wa soka wa mkoa wetu wa Kigoma kuwa Kocha Msaidizi Babi ameondoka ndani ya timu lakini taarifa hizo si za kweli, Babi bado yupo sana na tayari ameshaanza majukumu yake ndani ya timu.
“Kuhusu usajili tumeshaachana na wachezaji sita na tumebaki nao 17 ambao tulikua nao msimu uliopita lakini pia tumekamilisha sajili za wachezaji kadhaa ambao tutaweka kila kitu wazi muda ukifika.
“Msimu ujao tunahitaji kupanda Ligi Kuu hatutaki tena kubaki Championship na ndio maana tunafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda vizuri kwa upande wa usajili lakini pia maandalizi ya timu kuelekea msimu ujao wa mashindano hayo.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa