ALIYEKUWA kocha wa Polisi Tanzania, Malale Hamsin amefichua kuwa licha ya kuwa na ofa za klabu mbalimbali lakini ataweka wazi kila kitu baada ya mambo kukamilika.
Hamsini amefunguka kuwa “Kuna tetesi nyingi zinaendelea ambapo nimekua nikihusishwa kutua Mbeya City lakini pia JKT Tanzania lakini hizo zinabaki kuwa tetesi tu mpaka pale nitakapoweka kila kitu wazi.
“Nimepata ofa nyingi kutoka kwenye klabu mbalimbali japokua siwezi kuziweka wazi kwa sasa, nafikiri muda sahihi ukifika kila kitu kitakua wazi.
“Kwa sasa nipo mapumziko kwa muda mfupi kwetu Nzega huku Mkoani Tabora, lakini kabla ya dirisha la usajili kuelekea ukingoni tayari changamoto yangu mpya itakua imewekwa wazi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa