RAIS wa klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amefunguka kuwa hawakutumia gharama nyingi kumleta mchezaji huyo bali walitumia akili kubwa.

Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji watano waliosajiliwa kwenye kikosi cha Yanga katika dirisha kubwa la usajili ambalo linatarajiwa kufungwa Agosti 30, mwaka huu.

Akizungumzia hilo, Hersi amesema kuwa “Haijatumika hela nyingi kumpata Aziz Ki kama watu wanavyofikiria ni mikakati ambayo niliitumia ili kuweza kumpata mchezaji.

“Nilitengeneza mahusiano muda mrefu pia kuna ujanja ulitumika hata kuingia kwenye levo ya familia hata mama yake alikubali kumleta mtoto wake kucheza kwenye klabu yetu, pia alipata uthibitisho kutoka kwa mchezaji wetu Yacouba.

“Alikuwa amepewa ofa kubwa zaidi kuliko hapa Tanzania pia kulikuwa na klabu ya hapa nchini ilipeleka ofa kubwa zaidi yetu lakini alikubali kuja hapa kutokana na mazingira mazuri.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa