ALIYEKUWA kipa wa Coastal Union, kwa msimu wa 2021/22, Mussa Mbisa amejiunga na Tanzania Prisons kwa mkataba wa miaka miwili.

Licha ya majeraha aliyopata lakini Mbisa kwa msimu uliopita alifanikiwa kuonyesha kiwango bora ambapo alikuwa na Cleen Sheet saba.

Mbisa anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na Prisons baada ya dirisha hili kubwa la usajili kufunguliwa Julai mosi mwaka huu.

Wachezaji wengine waliosajiliwa na Prisons ni pamoja na Yusuph Mlipili, Amosi Isense, Mcha Hamis na Michael Masinda huku wakiachana na nyota wao 10.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa