HATIMAE wachezaji wa Yanga waliokuwa wakisubiriwa kambini ambao ni Shaban Djuma na Yannick Bangala tayari wamejiunga na kambi hiyo.
Yanga ilianza kambi yao rasmi ya kujiandaa na msimu wa 2022/23 Julai 22 mwaka huu, Avic Town huku nyota hao wakichelewa kuingia kambini.
Bangala, Djuma waongeza mzuka Yanga
Djuma
Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi jana ijumaa kilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp na kuibuka na ushindi wa mabao 5-1.
Baada ya nyota hao kuanza mazoezi leo jumamosi kwa sasa amebakia mchezaji mmoja kwa ajili ya kukamilisha idadi ya wachezaji wote wa msimu ujao ambapo kakosekana Benard Morrison.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa