Kocha mkuu wa Brazil Tite amefichua kuwa Barcelona iliitaka Brazil kuwa makini na Raphinha baada ya kuwapoteza wachezaji wanne kutokana na majeraha wakati wa mapumziko ya kimataifa.

 

Barcelona imeiomba Brazil kumchunga Raphinha

Jules Kounde, Ronald Araujo, Frenkie De Jong na Memphis Depay wamepata majeraha walipokuwa ugenini kuzichezea nchi zao. Raphinha alicheza dakika 80 za ushindi wa 3-0 wa Brazil wa mechi ya kirafiki dhidi ya Ghana Ijumaa na anaweza kukabiliana na Tunisia siku ya Jumanne.

Kocha mkuu wa Selecao Tite amesema Barcelona iliomba kazi ya winga huyo isimamiwe ili asije akaongezeka kwenye orodha ya wachezaji wenye majeraha.

Alisema: “Ili kuwe na uwazi wa hali ya juu, nawaambia leo wakufunzi wa Barcelona walizungumza na mkufunzi wetu wa viungo na kututaka kuwa waangalifu na Raphinha”.

 

Barcelona imeiomba Brazil kumchunga Raphinha

Barcelona ambayo ipo chini ya kocha mkuu Xhavi Hernandez wamewapoteza wachezaji wengi ambao wamepata majeraha akiwemo Araujo na kwa sababu hii wana wasiwasi wa kupoteza mchezaji mwingine, na waliulizia pia kama anaendelea vizuri.

Kalenda ya vilabu vikubwa ina msongamano mkubwa na hii inawatia wasiwasi kwani hadi watakapokutana kwa ajili ya Kombe la Dunia wachezaji watacheza michezo miwili kwa wiki, hicyo wanakuwa na wasiwasi kwani ligi inarejea wikendi ijayo na ushindani ni mkubwa.

 

Barcelona imeiomba Brazil kumchunga Raphinha

Raphinha ameanza mechi nne kati ya sita za LaLiga za Barcelona  msimu huu kufuatia uhamisho wake wa pesa nyingi kutoka Leeds United na alikuwa uwanjani kwa zaidi ya saa moja katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa