Klabu ya chelsea ya Chelsea imeachana na beki wake mwenye asili ya Brazil anayecheza timu ya taifa ya italia Emerson Palmieri.

Beki huyo wa kushoto aliejiunga na Chelsea mwaka 2018 akitokea As Roma amekua hana wakati mzuri sana ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kutopata nafasi ya kudumu ndani ya klabu hiyo.

, Chelsea Yaachana na Emerson., Meridianbet

Emerson Palmieri amejiunga na klabu ya West Ham kwa ada ya usajili ya euro milioni kumi na tatu na nyongeza ya euro milioni mbili.

Nyota huyo aliekua kwa mkopo klabu ya Olympique Lyon anaondoka Chelsea akiwa na cha kujivunia kwenye klabu hiyo yenye maskani yake jijini London amefanikiwa kushinda taji la michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya mwaka 2021, Uefa Europa league na mshindi wa pili wa Uefa super cup mwaka 2019 haya ni baadhi ya mafanikio ya mchezaji huyo ndani ya Chelsea.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa