Msimu Ligi Kuu ya Uingereza utaendelea pale tu, kila mchezaji atakapopimwa virusi vya Corona,” amesema Mtendaji Mkuu wa Chama cha Makocha kwenye Ligi(LMA) Richard Bevan.
Kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona Duniani kusimamishwa kwa Ligi nyingi ikiwemo EPL sasa kabla kurejea ni vyema kila mchezaji apimwe.
Lakini Richard Bevan amesema “vipimo vinatakiwa kwanza vipatikane kwa wafanyakazi wa NHS na wagonjwa.
“Hilo likifanyika, kwa namna yoyote tunaweza kuipata huduma hiyo kwenye michezo,”.
“Tutarejea uwanjani lakini afya ya mchezaji ni jukumu letu lazima tuunge juhudi za serikali kutokomeza Corona, hivyo ni muda wa sisi kuchukua tahadhari. Ni lazima kila mmoja apimwe kabla ya kurudi uwanjani,”

