Lewis Hamilton ameweka wazi baadhi ya vitu ambavyo angependa kuvifanya baada ya kustaafu mbio za magari F1. Amefanikiwa kukusanya mataji 6 ya michuano ya madereva hadi kufikia msimu uliopita.
Lewis ambaye ana miaka 35 anakaribia kufia mwisho wa kazi yake ya udereva wa mashindano huku vijana wengi wakiwa wamejiandaa kama kizazi cha washindi wajao.
Dereva huyu wa Mercedes haonekani kama ni mtu ambaye amechoka licha ya umri kusoge kiasi, na anasema huwa anakuwa ni mtu mwenye furaha sana pale anapokamatia usukani kuingia mashindanoni.
Michuano ya kutetea ubingwa wake wa sita kwenye mbio za magari imelazimika kusogezwa mbele kwa ajili ya mlipuko wa Virusi vya Corona, lakinin anatarajiwa kufanya vyema zaidi kuutetea ubingwa huo.
Katika ndoto ambazo anatarajia kutimiza baada ya kustafu soka ni kupandisha mlima mrefu zaidi duniani, mlima Everest. Mlima huu ni mlima mrefu zaidi wenye urefu wa mita 8,840 sawa na futi 29,029.
Pia katika orodha yake Lewis Hamilton vitu vingine ambavyo angependa kufanya ni kujifunza lugha, kwenda anga za juu na kutembea mwezini. Anatarajia kufanya haya akistaafu kazi yake ya soka!

