Inapotokea mchezaji anafanya vizuri hupewa hadhi yake anayostahili kwa mazuri anayoyafanya na kuonekana mbele za watu kwamba ni jambo kubwa na la pekee analifanya. Nafadi hiyo hutokana na mchango anaoutoa mchezaji husika ndani ya kikosi chake na matunda yanayotokana na uwepo wake na nafasi yake kuonekana wakati akiwa hayupo kwenye mchezo husika siku ya mechi.
Haya yamepata kutokea tayari kwa nyota wa klabu ya Chelsea, Hazard ambaye kutokana na mchango wake tayari watu wameanza kuuthamini na kumwona kuwa ni mkongwe wa klabu hiyo. Maneno hayo yametamkwa na aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo na nyota wa zamani wa klabu hiyo Drogba akiamini kwamba Hazard amefikia tayari heshima hiyo na anastahili kabisa kupewa heshima yake kama mkongwe.
Raia huyo wa Ubelgiji amekuwa akihusishwa na taarifa mbalimbali zinazomwonesha kwamba anataka kutimkia Madrid ili aweze kujiunga nao na kusakata soka la ukanda huo. Sababu nzima ya Madrid kumuhitaji ni kutokana na mchango wake wa wazi kwa klabu aliyopo na uwezo wakw kuwa wa juu sana na unaoonekana kukua kadri siku zinavyosonga mbele.
Maisha yake ya soka yalianzia pale Ufaransa katika klabu ya Lille ambapo tnamani yake ilianza kutambulika kwenye ulimwengu wa soka na kwamba anachokifanya ni kikubwa na cha pekee. Jambo lililopelekea mchezaji huyo kuonekana kwamba atafaa kwenye harakati za baadae ndani ya klabu ya Chelsea pale walipomsajili mwaka 2012 kwa ada ya £32m.
Hadi sasa kwa muda aliopata kuwa kikosini hapo ameweza kucheza jumla ya mechi 339 akiwa kama mchezaji wa Chelsea na katika mechi zake hizo tayari ameweza kufikisha magoli 105; ndani ya klabu hiyo. Ni uwiano mzuri sana wa magoli kwa mchezaji kama Hazard kuweza kufikia idadi hiyo. Na ni s3hemu ya historia kubwa sana kwake.
Hajaweza kuishia kucheza tu idadi hiyo ya mechi na kufunga magoli hayo pekee. Pia, ameweza kutwaa vikombe akiwa na klabu hake hiyo; ambapo mara nyingi mataji kama hayo huwa ndiyo heshima kwa mchezajj yoyote anapochukua mataji. Kwake ameweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara mbili, kombe la Europa, kombe la FA na kombe la ligi.
Akizungumza na wanahabari nyota mwenzake aliyewahi kuhudumu kikosini hapo, Drogba anasema uwezo wa Hazard tayari umeshaandikwa kwenye vitabu vya klabu hiyo na ni suala ambalo nyota huyo anastahili kabisa kutokana na mchango wake aliouonesha klabuni hapo. Na anastahili kabisa nafasi hiyo adhimu kama mkongwe.
Wakati mwingine sifa kama hizi huchangia mchezaji kushuka kiwango chake cha awali kutokana na kuridhika kwamba ana upekee ambao wengi wanamwona kwamba anao. Hivyo, ili azidi kujijengea heshima hana budi kujiimarisha na kuendelea kuijenga historia yake ili kuonekana zaidi ya alipo.

