Hawaijui Tuzo ya Mwezi Uingereza

Furaha ya mchezaji siku zote ni kushinda vikombe na mataji mbalimbali ambayo huweza kumwonesha kwamba anafanya kitu ambacho kinatambulika na kinaonekana na wengi wanaotambua thamani ya soka duniani. Jambo hilo ndilo huchochea ubunifu uwanjani kwa mchezaji mmojammoja hadi ngazi ya timu.

Leo tunakuletea majina ya wachezaji ambao wanafanya vizuri na waliwahi kufanya vizuri lakini hawajabahatika kabisa kuitwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ndani ya ligi ya Uingereza; kitu ambacho sio rahisi kuakiamini, lakini ndiyo uhalisia wenyewe katika soka na ni kitu ambacho kwa nafasi fulani hakipingiki kutokea.

Peter Schmeichel

Aliweza kushinda medali zaidi ya nne na United katika kipindi cha mwaka 1998/99 akiwa ni sehemu ya chachu kubwa kwa kikosi hicho kutwaa ubingwa wa ligi. Kwa wakati wote kikosi hicho kilikuwa chini ya mzee Alex lakini bado alishindwa kudhihirisha ubora wake hadi kutwaa tuzo hiyo pamoja na kuonesha uwezo mkubwa.

David de Gea

Mchezaji wa misimu mingi sana ndani ya United akiweza kuzoa tuzo nyingi kwa nafasi yake. Akiwa na kombe la ligi, ligi kuu, ngao ya jamii na FA lakini kama haitoshi alishinda tuzo ya kuokoa mpira hatari ambayo kwa msimu mzima hakuonekana mwingine zaidi yake lakini hiyo haikutosha kumpa heshima hiyo aweze kuwa kama mchezaji bora wa mwezi ndani ya ligi.

Vincent Kompany

Mchezaji huyo wa Manchester City alikuwa mhimili mkubwa sana chini ya kikosi hicho kwa vipindi vilivyopita na hivi vilivyopo katika siku za hivi usoni; lakini pamoja na hilo hajawai fanikiwa kutwaa tuzo ya kuwa mchezaji bora angalau hata kwa mwezi mmoja ndani ya ligi hiyo ambayo ana historia nayo.

Patrick Vieira

Wengi hawawezi kusahau au kujifanya kusahau jina hilo kutokana na makubwa aliyofanya akiwa na kikosi cha timu ya taifa Ufaransa na klabu ya Arsenal. Pamoja na kuwa na mengi ameyafanya na kikosi hicho lakini hajafanikiwa kabisa kupewa nafasi ya kuimiliki tuzo hiyo kubwa kabisa ndani ya taifa la Uingereza.

Didier Drogba

Mchezaji mwenye jina kubwa ndani ya Chelsea ambaye hata sasa klabu hiyo bado inatamani angeendelea kuwepo. Kiatu cha dhahabu, kuhusishwa ndani ya kikosi cha kinachounda wachezaji kwa mwezi, kufikisha idadi kubwa ya magoli kwenye ligi na kuhusika kwake ndani ya klabu bingwa, lakini hajawai kabisa kupitiwa na bahati ya kuwa mchezaji bora wa mwezi akapata tuzo kwa kutokana na hilo.

Acha ujumbe