Hasara Kubwa Yaikumba Chelsea Licha ya Mapato Kuongezeka

Klabu ya Chelsea FC imetangaza kupata hasara kubwa ya kabla ya kodi ya pauni milioni 262.4 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2025, ikiwa ni rekodi mpya ndani ya Premier League.

Hasara Kubwa Yaikumba Chelsea Licha ya Mapato KuongezekaHasara hiyo imevunja rekodi ya awali iliyowekwa na Manchester City ya pauni milioni 197.5 katika msimu wa 2010/11. Hata hivyo, Chelsea walipata faida ya pauni milioni 128.4 mwaka uliopita, iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na uuzaji wa timu ya wanawake kwa kampuni tanzu ya Blueco Midco kwa karibu pauni milioni 200.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, hasara hiyo imetokana kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji katika msimu wa 2024/25 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Hasara Kubwa Yaikumba Chelsea Licha ya Mapato KuongezekaChelsea pia iliripoti mapato ya pauni milioni 490.9, ikiwa ni ya pili kwa ukubwa katika historia ya klabu hiyo, yakiwemo mapato yaliyotokana na ushindi wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu mwaka uliopita.

Mwezi uliopita, klabu hiyo ilikiri kukiuka kanuni za ligi kuhusiana na malipo yasiyofichuliwa yenye thamani ya pauni milioni 47.5 yaliyofanywa chini ya mmiliki wa zamani Roman Abramovich.

Hasara Kubwa Yaikumba Chelsea Licha ya Mapato KuongezekaKutokana na ukiukwaji huo, Chelsea ilitozwa faini ya pauni milioni 10.75 na kupewa adhabu ya kusimamishwa kusajili wachezaji kwa mwaka mmoja, ingawa adhabu hiyo ilisimamishwa kutekelezwa.

Premier League ilieleza kuwa klabu hiyo ilinusurika adhabu ya kupokwa alama kutokana na ushirikiano mkubwa waliouonesha wamiliki wapya wakiongozwa na Todd Boehly, ambao walijiripoti wenyewe kuhusu taarifa zilizoanzisha uchunguzi.

Hasara Kubwa Yaikumba Chelsea Licha ya Mapato KuongezekaAkizungumzia hali hiyo, taarifa ya ligi ilieleza “Chelsea walionesha ushirikiano wa kipekee katika mchakato mzima wa uchunguzi, jambo lililochangia maamuzi ya mwisho kutotolewa kwa adhabu kali zaidi.”

Pamoja na hasara hiyo, Chelsea ilizingatiwa kufuata kanuni za faida na uendelevu (PSR), ambazo huruhusu klabu kupata hasara ya hadi pauni milioni 105 ndani ya kipindi cha miaka mitatu, huku baadhi ya matumizi kama yale ya timu za wanawake na maendeleo ya vijana yakiondolewa kwenye hesabu hizo.

Hasara Kubwa Yaikumba Chelsea Licha ya Mapato KuongezekaKwa upande mwingine, timu ya wanawake ya Chelsea, mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake kwa misimu mitatu mfululizo, ilitangaza hasara ya pauni milioni 17.1 licha ya kuingiza mapato ya pauni milioni 21.3.

Akihitimisha, taarifa ya klabu ilieleza “Licha ya changamoto za kifedha, tunaendelea kujenga msingi imara wa maendeleo ya muda mrefu ndani na nje ya uwanja.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.