Kocha wa klabu ya AS Roma Jose Mourinho ameibukuwa kuwa chaguo namba moja la kumrithi kocha wa klabu ya PSG Mauricio Pochettino ambaye muda wowote anaweza kufungashiwa virago na matajiri wa klabu hiyo.
Kulingana na taarifa zinazosambaa mitandaoni barani ulaya kuwa mabingwa wa Ligue 1 wanaona kuwa Jose Mourinho ndio chaguo sahihi kuchukua mikoba ya Pochettino, Kocha huyo mwenye asiri ya argentina kuondoka kwake kwenye klabu hiyo ni swala lisiro epukika kwani kwani mabosi wa klabu hiyo wamepanga kufanya maboresho makubwa kwenye klabu hiyo.

Mwezi uliopita walifanikisha kumbakisha nyota wa klabu hiyo Mbappe na kumuondoa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Leonardo, na kumuajiri Luis Campos ikiwa ni moja ya maboresho ya klabu hiyo, huku maamuzi ya Al Khelaif ni kumfukuza Pochettino baada ya kushindwa kuchukua ubingwa wa Ulaya.
Luis Campos ni moja ya watu wa karibu wa Jose Mourinho baada ya kufanya kazi pamoja kwenye klabu ya Real Madrid, kuwepo kwa Campos kwenye viunga vya Parc des Princes kuna toa mwanga kwa Mourinho kuweza kufanya kazi kwenye klabu hiyo.
Jose Mourinho amekuwa kocha wa kwanza kwenye historia ya Ulaya kufanikiwa kuchukua maombe yote makubwa ya Ulaya yanayoandaliwa na shirikisho la mpira wa miguu barani ulaya, na pia ameweka rekodi ya kuwa kocha pekee aliye shinda michezo yote ya fainali ya ulaya akiwa kama kocha.
Kwa sasa itakuwa kazi ngumu sana kwa klabu ya PSG kuweza kumshawishi kocha huyo ajiunge na klabu hiyo, sababu amepewa uhuru zaidi kwenye klabu hiyo pia amekuwa maarufu ndani ya klabu hiyo baada ya kuiongoza kuchukua ubingwa wa kwanza wa ulaya na kombe la kwanza ndani ya miaka 14.
Jose Mourinho ikiwa atachagua kwenda kuifundisha klabu ya PSG, itakuwa mara ya pili kwenda kubeba mikoba ya Pochettino, awali alichukua kijiti cha Pochi kwenye klabu ya Tottenham baada ya kufungashiwa virago.
Pochettino anafukuzwa baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja tu, na kufanikiwa kuwapa ubingwa wa ligi kuu ya Ufaransa, lakini kipaombelea cha matajiri wa PSG ni ubingwa wa Ulaya.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!


