BAADA ya kurejea mazoezini, Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amefunguka kuwa ataendelea na staili yake ya kutetema hivyo tabu itakuwa pale pale.

Mayele ni miongoni mwa wachezaji waliochelewa kuingia kambini Avic Town, Kigamboni kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23.

Akizungumzia maandalizi yao, Mayele amesema kuwa “Nimerudi kambini na tumeanza kujiandaa na msimu mpya nina hamu sana ya msimu ujao kwahiyo siwezi kubadilisha staili yangu ya kushangilia

“Tutaendelea kutetema kama tulivyokuwa tunafanya kwa msimu uliopita tabu ipo pale pale.

“Ni kweli timu zilinifuata lakini mimi ni mchezaji halali wa Yanga na nilisaini mkataba wa miaka miwili hivyo kwa sasa umebakia mmoja.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa