Mkuregenzi wa michezo wa klabu ya Sevilla Monchi ameilaumu klabu ya chelsea kwa kushindwa kufanikisha uhamisho wa beki wa kati wa klabu hiyo ambaye amesajiriwa na Barcelona.

Klabu ya Chelsea walishafanya makubaliano na klabu ya sevilla kwa ajiri ya uhamisho wa Kounde ambapo kiasi cha £55million kilikuwa tayrai kwa ajiri ya malipo huku makubalilano na mchezaji husika yalishakamilika kabla hata ya Barcelona kuingilia kati na kufanikiwa kumsainisha mchezaji huyo.

Sevilla, Sevilla Yailaumu Chelsea kwa Jules Kounde, Meridianbet

“Mwanzoni kwenye ufunguzi wa dirisha la usajiri kulikuwa na offer nyingi kuliko mwishoni, vilabu vingi vilikuwa vinamuhitaji, mwishowe Chelsea walikuwa na juu ya wote, tulifanya mazungumzo mwezi uliopita hadi tulipofikia makubaliano ya mdomo Alhamisi iliyopita.

“Mchezaji pia alifikia makubalilano lakini kipindi cha mwishoni, chelsea walikuwa na wasiwasi. Kila kitu kilisimama, walikuwa na offer nzuri lakini waliamua kuacha.

“Mara ya kwanza Alemany anawasiliana na mimi ilikuwa jumatatu na Barca walielezea hitaji lao kwetu. Tuliwauliza offer yao kwanza, ilikuwa ndogo na ile ambayo tulikuwa nayo kichwani lakini hatimaye walikuja na kiasi kilichovutia na Offer kubwa kwenye historia ya Sevilla.” Alisema Monchi

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa