Kuna ambae hapendi ule mchezo wa kizamani wa kumaliza mpira kwa Masumbwi na vurugu za kusukumana? mtindo huu umekua unafurahiwa hata na wachezaji wenyewe wanapokutana uwanjani, na wengi hua hawezi kabisa kujizuia. Hapa nitakushushia matukio matatu yaliyosababisha mechi kuisha kabla ya muda wake au kuisha kwa muda wake na kumalizika kwa vurugu kweye matukio ya kimichezo.
Lee Bowyer dhidi ya Kieron Dyer, 2005
Turudi nyuma mpaka mwaka 2005 kwenye ligi kuu ya Uingeleza iliyowakutanisha Newcastle na Aston Villa, ambapo wawili hao walitolewa nnje wote kwa kosa la kutupiana Makonde wenye kwa wenyewe wakiwa ni wachezaji wa timu moja,

West Browich Albion dhidi ya Fulham, 2004-05
Hii ilitokea msimu wa 2004-05 ambako West Bromwich Albion walifanikiwa kuchukua nafasi yao katika ligi kuu licha ya kua wa mwisho kipindi cha sikukuu za Christmass . ilikua ni mara ya kwanza kwenye kombe la premiership kutokea.uwanja ulijaliwa na mashabiki walio jawa na furaha iliyotokana na ushindi huo wa West Bromwich.

Manchester United dhidi Arsenal, 2003
Ni wazi kwamba vugu vugu la kuvurugana baina ya timu hizi zilianzia kwenye korido ya njia zinazotoka kwenye vyumba vya kubadirishia nguo. Ambako Patrick Viera alifanya kosa kubwa la kukatiza kwa fujo kwenye mstari waliosimama wachezaji wa Manchester United, yani kama asingokuepo mtu wa ulinzi basi angeweza hata Kumwangusha Roy Keane
Mbaya zaidi ni pale mshambuliaji wa Manchester United Ruud van Nistelrooy alishinda pernaty huku wachezaji wa Arsenal wakisema alijiangusha makusudi.

matukio ya vurugu yamekua kwa namna kubwa sana yakiwa yana Athili Matokeo katika soka na ukizingatia soka ni mchezo wa kiungwana, inashauriwa kuacha kabisa kujihusisha na michezo isiyo ya kiungwana kwenye soka.


Povel
Gud news