Klabu ya AC Milan ilifikia makubaliano binafsi na Divock Origi mwezi moja uliyopita na sasa inasubiriwa kusaini mkataba tu ambapo atatua klabuni hapo kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Liverpool kuisha.

Mpango umethibitishwa kwamba atafanya vipimo wiki ijayo kisha atakuwa tayari kusaini mkataba na mabingwa hao wapya wa Serie A.

Ripoti zinadai kwamba Origi anaelekea kusaini mkataba wake na Milan baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool na Real Madrid ambayo itakuwa ni mchezo wake wa mwisho kwa Reds. Kikwazo cha mwisho kilikuwa uwezekano kwamba kifungu kipya kinaweza kuanzishwa baada ya kufikia idadi fulani ya mechi kwa msimu inaonekana kuwa hakuna tatizo tena.

Uhamisho wa Origi hautakuwa kama Olivier Giroud ambaye alitua klabuni hapo akitokea Chelsea dirisha lililopita ambapo Milan walilazimika kulipa tokeni ya ada ya uhamisho licha ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kumaliza mkataba na The Blues.


 

VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa