Nahodha wa timu ya Borussia Dortmund,Marco Reus amefurahi kwamba Jadon Sancho ataendelea kusalia Dortmund kwa msimu mmoja zaidi, wakati Manchester United ikionekana kusanda katika harakati za kumnasa kiungo mshambuliaji huyo.
United walikuwa wakivutiwa na kumsajili Sancho ilikuimarisha nguvu ya kikosi chao lakini hakuna siri, Dortmund walikuwa wakitaka kiasi cha Euro milioni 120 (£108m) ilikumuachia Sancho.
Sancho yupo kwenye mkataba mpaka 2023 na Reus amefurahishwa kuendelea kucheza pamoja na mchezaji huyo wa zamani wa timu ya vijana ya Manchester City katika dimba la Iduna Park.

“Kwetu ni jambo kubwa. Tunafuraha kwamba tutaendelea kuwa naye walau mwaka mmoja,” Nahodha wa BVB Reus aliwaambia maripota. ” Ndiyo kwa sababu bado anaendelea na ksi yake ya kutengeza asisti za magoli na kusumbua ngome ya upinzani tutapata alama nyingi.
Reus hakuwa tayari kusema kama Sancho anaweza kufika kiwango cha uchezaji kama cha kina Lionel Messi na Christiano Ronaldo.
“Ni mchezaji mzuri sana katika timu yetu na huenda siku moja atakuja kuwa mchezaji mkubwa kama wachezaji wawili [Messi na Ronaldo] tutaona.
“Anahitaji muda na uzoefu lakini pia kuna wakati mambo huwa hayaendi poa lakini akiwekeza bidii na kujituma atafika sababu anakipaji kikubwa.
Sancho alifunga goli 17 msimu uliyoisha nyuma ya Thomas Muller (21), Timo Werner (28) na Robert Lewandowski (34) na kuwa ni mchezaji pekee aliyetoa asisti nyingi asisti 16 katika Bundesliga.
Dortmund itawakabili Bayern Munich katika michuano ya German Super Cup siku ya Jumatano, huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa goli 2-0 na Augsburg katika Bundesliga siku ya Jumamosi.
Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!
Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!


felister
ni Jambo jema
Saupha mohamed
Safii
Mwajumah
Ni jambo zuri
magdalena
dortmund wanamuhitaji sana sancho ndo maana ata kuondoka wanamuwekea ugumu
Elika
Naona ni bora akaendelea kulisongesha hapo hapo
Adelta
Ni vizuri abaki tu hapo
Sauda
Sancho, mpira anautendea haki kwa kweli.
Nasra
Nice
Fatina mfigi
Abaki tu hapo
Zeiyana
Dortmund hawezi kumuuza Sancho ndio tegemezi lao kubwa kikosoni pale
Mwanahamisi
Abaki tuu
Dorophina
Bora sancho walivyomuongezea muda wa kuendelea kuitumikia Dortmund naona bado wanaona umuhimu wake
Caroline
Sancho ataimarisha nguvu ya kikosi
Latifa juma mohamed
Vizuri zaidi.
Hopemwaikuka
Tulia hapo hapo tu
Asia Abdy
Waooh safii
Shani
Sancho ni matata San na kubaki dortmund ni sahihi
Johnmary joel
Ni mchezaji mzuri na pia maamuzi mazuri #meridianbett
aisha
Man u iachane nae kuna wachezaj wazur t sokon sio kwa bei hiyo
Khadija
Jambo ni jema
Angelina
Safi
Gabriel
Sancho ndio tegemezi lao kubwa
Sadick
Hilo linaongeza ugumu kwa Man U kumusajiri Jadon Sancho#meridianbettz
Issa
Mtu hatari dortmund reus hafai
Amiri Kayera
Kama team inamuitaji Kwa ili kufany vzr msim ujao
Sabrina
Nilijua Dortimund sio rahisi kumuachia sancho kizembe hivyo
Rehema
Good
farida ahmadi
Sancho Yuko vizuri
Lydia Emmanuel Magoti
Kipige dogo apo apo Man U naona wamesanda kumwaga pesa juu yako
Tatu
Ni ngumu sana dortimund kuachia sancho bado wanamuitaji
Ernest
Hapa kuna vitu viwili, sidhani kama Sancho kuendelea kubaki Dortmund ni uamuzi sahihi sana kwake kwa kipindi hiki maana ukiangalia deal la Man U ni deal zuri au Sancho binafsi hapendi soka la Uingereza??
David Pere
United walikuwa wakivutiwa na kumsajili Sancho ilikuimarisha nguvu ya kikosi chao lakini hakuna siri, Dortmund walikuwa wakitaka kiasi cha Euro milioni 120 (£108m) ilikumuachia Sancho.