Stephen Akwari: Mabingwa Humaliza Walichokianza

Stephen Akwari Hajamaliza mbio lakini Mamo Wolde wa Ethiopia alishamaliza kilometa zake 42, alishachukua medali yake ya dhahabu, labda alikuwa amejipumzisha hotelini akifikiria shangwe za mapokezi yake atakaporudi nyumbani Ethiopia.

Ilikuwa jioni sana na muda ulishakwenda, sherehe zilishatamatika na uwanjani Estadio Olympico Universitario walikuwa wamebaki watu wachache sana waliosalia baada ya kuhitimisha Olympic za 1968, Mexico City.

Ndipo alionekana mwanariadha mmoja akiingia uwanjani, mguu wake wa kulia umeufungwa bandage, anatembea kwa shida akichechemea. Alitembea kwa tabu hadi katika mstari wa kumaliza kisha akapita zake kumaliza mbio. Alikuwa ni John Stephen Akwari kutoka Tanzania.

Stephen Akwari
Stephen Akwari
Wakiwa katikati ya mbio kama kilometa 30 hivi, Stephen Akwari alidondoka vibaya baada ya kugongana na mwenzake, akatenguka mguu wa kulia na bega.

Badala ya kuamua kuacha na kuondoka, Akwari alienda akapatiwa matibabu, kisha akarudi kuendelea na mbio akiugulia maumivu mpaka alipomaliza.

Alimaliza nafasi ya 17 kati ya wanariadha 17 waliomaliza, Wanariadha 54 waliishia njiani baada ya kuona hawawezi kushinda tena. Lakini Akwari hakujali ushindi sana, alichojali ni kumaliza. Alitumia masaa matatu na dakika 25, kumbuka bingwa alitumia masaa mawili na dakika 20.

Akwari alipokatiza mstari wa kumaliza, uwanja ulilipuka kumshangalia. Mwandishi mmoja alimuuliza kwanini alichagua kuendelea kukimbia akiugulia maumivu makali ilihali alijua hawezi kushinda tena??

Akwari alimpa kauli ambayo mpaka leo inabaki kuwa kauli bora zaidi ya kimichezo kuwahi kusikika. Akwari alimuambia, “My country did not send me 5,000 miles to start the race; they sent me 5,000 miles to finish the race.”

Tafsiri yake ni kuwa “Nchi yangu haikunituma maili 5,000 nije kuanza mbio, Walinituma maili 5,000 nije kuanza na kumaliza” Kwasababu ya ule ushujaa, mpaka Leo Stephen Akwari yupo kwenye kitabu cha heshima cha Olympic.

Katika kila unachokifanya, kazana kukimbia mbio zako. Usijali changamoto unazopitia, usijali kama utashinda au la, usijali wenzako wamefika wapi, kazana kukimbia mbio zako na kuzimaliza.


SHINDA NA TIKI REWARD KASINO

Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!

Tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 Komentara

    Ni kweli

    Jibu

    Ni kweli

    Jibu

Acha ujumbe