Erik ten Hag anasema hajutii kuchukua maamuzi ya kufanya kazi Manchester United badala ya kusubiri kuona kama alikuwa mgombea kuchukua nafasi ya Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City.

 

Ten Hag Hajutii Kuwa Man Utd.

Guardiola, ambaye alifanya kazi na Ten Hag katika klabu ya Bayern Munich, alidai mwezi Aprili kwamba Mholanzi huyo ‘angeweza kuwa ndiye’ wa kumrithi pale Etihad.

Wakati watu hao wawili wakijiandaa kumenyana katika mechi ya Manchester derby kwa mara ya kwanza Jumapili, Ten Hag alisisitiza kuwa anafurahishwa na uamuzi wake wa kuondoka Ajax na kujiunga na United majira ya joto.

 

Ten Hag Hajutii Kuwa Man Utd.

“Hiyo ni pongezi nzuri,” alisema. “Lakini nilishawishika kwa asilimia 100 kuchagua Man United, ikiwa na kila kitu ndani yake. Sikujuta hata sekunde moja.”

“Namkubali sana Pep Guardiola kwa sababu sio tu kwamba hana mafanikio, anafanya kwa namna fulani ambayo inawavutia sana watu kwenye soka, hiyo ni zawadi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa