Trevoh Chalobah mchezaji wa klabu ya Chelsea ana uwezekano mkubwa kutolewa kwa mkopo kumpisha Wesley Fofana kutoka klabu ya Leicester City. Chelsea ipo mbioni kukamilisha dili la beki huyo wa kifaransa anaeitumikia klabu ya Leicester ya City.

Chelsea imepanga kumuachia beki huyo kijana waliompandisha kutoka shule yao kukuza vipaji maarufu kama Cobham kwa mkopo kuelekea klabu ya Red Bull Leipzig ya nchini ujerumani.

trevoh chalobah, Trevoh Chalobah kumpisha Fofana., Meridianbet

Chelsea wanapambana sokoni kuhakikisha timu inakua imara kwani mwalimu Thomas Tuchel anaonesha kutoridhishwa na sajili ambazo amezifanya kwenye majira haya ya joto kwani anahitaji watu bado kwenye kikosi ndo maana bado yupo sokoni kupambania saini ya beki ya Leicester City Wesley Fofana ambae atatoa nafasi kwa kijana Chalobah kutolewa kwa mkopo.

Chelsea kwa miaka ya karibuni wamekua wakiwatoa vijana wao kwa mkopo waliofuzu kwenye shule yao ya vijana ili wapate kupata uzoefu na kuja kuisadia timu hiyo mbeleni na Trevoh Chalobah anakua miongoni mwao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa