Mkali na mkongwe wa mbio za pikipiki Valentino Rossi mwenye umri wa miaka 42 leo rasmi amestaafu mchezo huo baada ya kuutumikia zaidi ya miaka 26 akishinda mataji mbalimbali ikiwemo ya dunia ya mbio za pikipiki
Mkongwe huyo amestaafu katika mbio za leo zilizofanyika kwenye jiji la Valencia nchini Uhispania Rossi ambaye ni raia wa Italia amemaliza katika nafasi ya 10 kati ya waendesha pikipiki wengi walioshiriki mbio hizo

Mkali huyo ambaye anatajwa kuwa mmoja wa waendesha vyombo vya moto bora kuwahi kutokea yupo katika orodha moja na wakali wengine akiwemo mkali wa langalanga Michael Schumacher,Ayrton Senna na Mick Doohan
Mpaka anastaafu leo Valentino Rossi amecheza ama kukimbia mbio 432 ,akishinda mbio 115 sambamba na kunyakua mataji tisa kwénye mchezo huo.
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.