Nyota wa PSG, Marco Verratti huenda akawa ametania kusema kuwa karantini kunampa mda zaidi wa mazoezi.
Kama maastaa wengine, nyota huyu naye yupo karantini kwa toka ligi iliposimama kwa ajili ya kujiweka salama. Kwa sababu ya kuhofia wachezaji wanaweza wakarejea wakiwa wamepotea kwenye fomu, basi kila mtu anafanya jitihada zake za mazoezi.
Verratti amekuwa msaada kwa PSG kusimama kileleni akishirikiana na mastaa wengine wa klabu hiyo. Staa huyu anasema anajiweka bize sana karantini na kutumia mda wake kwa mazoezi kuhakikisha kuwa hapotei mchezoni.

Hata hivyo, biola shaka mazoezi yana vipengele tofauti na kuna wakati unahitaji watu ili kukamilisha uhalisia wa mazoezo kama vile kukabana na mbinu nyingine nyingi, ni tofauti na unapokuwa karantini peke yako unafanya mazoezi. Bila shaka staa huyu aliweka utani kidogo katika kusisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi wanapokuwa karantini ili wasijekuta mwana si wao wanaporejea dimbani.

