Wanaofanya Vizuri Katika Safu za Ulinzi

Kwa kadri siku zinavyosonga mbele majukumu ya ulinzi nayo yamekuwa yakibadili mwekekeo wake kutoka katika hali iliyokuwepo hapo awali ya kwamba kazi mabeki ni kulinda na kuzuia mipira isiweze kupita kuelekea katika himaya yake; lakini mambo hayo yamekuwa tofauti kwa sasa ambapo pia safu hizo hupaswa kushambulia au kuanzisha mashambulizi.

Kuna baadhi ya wachezaji katika safu hiyo wamekuwa na matokeo mazuri sana ambayo yamechangia wao kuweza kuzifanya klabu zao kung’aa kimatokeo na hata kiuchezaji. Baadhi ya vikosi ambavyo vimeonekana kufanya vizuri kwa siku za usoni vimechagizwa na wachezaji hao ambao wamefanya makubwa, wakiweko:

Jordi Alba

Barcelona walijivunia kuwa na mchezaji huyo ndani ya kikosi chao kutokana na namna ya uchezaji wake akiwa katika nafasi hiyo ya ulinzi. Ni miongoni mwa walinzi wenye uwezo mkubwa wa kupandisha mashamhulizi na kasi kubwa ya kurudi kukaba pale timu inaposhambuliwa. Kwa mfumo wa klabu hiyo ambayo uhai wake wa timu upo sana katikati huhitaji walinzi ambao wana uwezo wa kupanda na kushuka kwa kasi sana ili kuongeza nguvu.

Dani Carvajal

Tangu atue kikosi kwake mwaka 2013 alikuwa sukari sana ndani ya kikosi hicho. Uwepo wake umekuwa chachu ya kufanya kikosi kiweze kuwa na nguvu ya kushambulia muda mwingi; hasa ikirejewa nyuma aliweza kuhusika kwa kiwango kikubwa katika upatikanaji wa magoli mengi yaliyofungwa na Ronaldo kutokana na uwezo wake. Kutokufumania nyavu kwake hakumfanyi aomekane hana ubora, bali ni kutokana na nafasi anayohusika nayo.

Andrew Robertson

Raia huyo wa Scotland tangia asajiliwe kutokea Hull City ameweza kukaa vyema ndani ya mfumo wa Klopp akishirikiana na walinzi wenzake. Miongoni mwa vitu vya msingi alivyovifanya kwa hivi karibuni kwa aina ya uchezaji wakevinamvutia kila mmoja anayemtazama mchezaji huyo. Ametoa pasi sita za magoli  ndani ya ligi hadi sasa na mbili ndani ya michuano ya klabu bingwa ya Ulaya.

Joshua Kimmich

Guardiola aliweza kuutambua uwezo wa mchezaji huyu miaka ya 2015 alipokuwa mwalimu ndani ya kikosi hicho. Ni uzao wa kijerumani ambao unategemewa kuja kuleta mapinduzi makubwa ya kisoka ndani ya taifa hilo kubwa na klabu yake ya Bayern. Hadi sasa ana pasi za magoli 10 na zile za kombe la ligi ya mabingwa Ulaya ameweza kuchangia upatikanaji wa magoli mawili. Katika umri wake miaka 24 anaonekana kuwa na mwenendo mzuri sana ndani kikosi hicho na hata popote atakapojiunga.

Acha ujumbe