Simba SC baada ya kumtambulisha nyota wao, Nelson Okwa, Uongozi wa wa klabu hiyo umefunguka kwamba amebaki mchezaji mmoja anayecheza kwenye nafasi ya straika kwa ajili ya kufunga usajili wao.

Okwa ambaye anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji alitambulishwa na
Simba jana jumatano usiku kwa mkataba wa miaka miwili.

Simba SC

Akizungumzia usajili huo, Ofisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa
“Tunayo furaha kumtambulisha mchezaji wetu Nelson Okwa. Atajiunga na
kikosi Dar.

“Kikosi baada ya kutua Dar wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja
na kesho wataingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na siku ya Simba.

“Hatujaishia hapo kwenye usajili lakini ndani ya wiki hii
tutamtambulisha tena mchezaji mwingine ambaye anacheza kwenye nafasi za
mbele ili kuziba nafasi zilizopo.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa