Mchezaji wa kimataifa wa Uganda anayecheza kwenye klabu ya Yanga Khalid Aucho ameahidi kuwa kuelekea msimu ujao wanatarajia kufanya vizuri kwenye ligi na michuano ya kimataifa.

Aucho kwenye msimu uliopita alichezea  Yanga michezo 21 na kufanikiwa kufunga bao moja na kutoa asisti tatu kwenye michezo yote aliyoicheze klabu hiyo.

Yanga, Khalid Aucho Aahidi Jambo Yanga, Meridianbet

“Msimu uliopita hatukuwa fiti sana ndio maana hata kwenye michuano ya
kimataifa tulitolewa katika hatua ya awali.

“Msimu ujao tunawaahidi wana yanga kwamba tutafanya vizuri kutokana na
maandalizi ambayo tumefanya hata kama ni kwa kipindi hiki kifupi ambacho
tumejiandaa kinatosha sana.

“Wachezaji ambao wameongezwa kwenye kikosi wataongeza kitu na
tutafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa