KIKOSI cha Azam FC, kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa ligi dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Septemba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka zakazi’ amesema timu hiyo inaendelea kujifua kwa ajili ya mchezo wao ujao wa ligi.

 

Azam Waiwinda Mbeya City

“Timu yetu inaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City lakini baada ya hapo pia tutakuwa na mchezo wetu wa kimataifa.

“Kikosi kitaondoka Septemba 29 mwaka huu kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo na wachezaji wote wapo fiti.

 

Azam FC
Azam FC

“Kwa sababu kocha amekuja wakati ligi tayari imeanza kwahiyo anaendelea kuingiza taratibu falsafa zake kwa ajili ya kuhakikisha malengo ya timu kwa msimu huu yanatimia.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa