Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania imesema kuwa ipo kwenye hatua za kutekeleza ujenzi wa uwanja wa michezo Jijini Dodoma ambayo uwanja huo utagharimu kiasi cha pesa za Kitanzania Shilingi Bilioni 420.

Dodoma:Bilioni 420/=Tsh Kujenga Uwanja

Mbunge wa Morogoro Kusini Mhe, Innocent Edward Kalogelisi, aliuliza ni lini ahadi ya ujenzi wa Uwanja wa Mpira Jijini Dodoma, iliyotolewa na Mfalme wa Morocco itatekelezwa?.

Dodoma:Bilioni 420/=Tsh Kujenga Uwanja

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul alisema kuwa:

“Serikali imefuatilia utekelezaji wa ahadi ya ujezi wa Uwanja wa Mpira Jijini Dodoma, Iliyotolewa na Mfalme wa Morocco, Mawasiliano ya Utekelezaji wa mradi huo, baina ya Serikali ya Tanzania na Morocco bado yanaendelea”.

“Vilevile katika kuhakikisha kwamba mradi huu unatekelezwa, Serikali imedhamiria kutafuta fedha kutoka vyanzo mbalimbali vikiwemo sekta binafsi na wabia wa Maendeleo”

Dodoma:Bilioni 420/=Tsh Kujenga Uwanja

Mhe, Innocent pia alihoji, ni kwanini Serikali isitaje ni lini haswa wataanza ujenzi huo, mbali na kusema wanatafuta wabia wa maendeleo, na majibu ya Naibu Waziri wa Michezo Pauline Gekul yalikuwa ni kama ifuatavyo:

“Serikali imekwisha kujipanga, ndiyo maana tumekwisha fanya upembuzi yakinifu, kujua kwamba huu uwanja tunaujenga wapi, na unahitaji gharama kiasi gani, huu uwanja unahitaji zaidi ya Shilingi Bilioni 420, na Serikali tupo kwenye hizo hatua pamoja na maongezi yanayoendelea lakini tunaendelea kutafuta pesa”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa